BAADHI YA
MASHABIKI WA COASTAL UNION WAMEAMUA KUCHUKUA UAMUZI WA KUANDIKA BARUA
KUUSHITAKI UONGOZI WA KLABU YAO KWA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF).
UAMUZI WA
MASHABIKI HAO, WAKIONGOZWA NA KATIBU WAO ABDULLATIF OMAR FAMAU UMETOKANA NA
UAMUZI WA KATIBU MKUU WA COASTAL UNION, KASSIM EL SIAGI KUWAZUNGUSHA KUHUSU
KUPATA UANACHAMA.
FAMAU
AMESEMA WAMEKUWA WAKIFANYA KAZI YA ZIADA KUPATA UANACHAMA LAKINI EL SIAGI
AMEKUWA AKIWAZUNGUSHA.
KATIKA
BARUA HIYO AMBAYO SALEHJEMBE IMEINASA, INAELEZA KILA KITU KUHUSIANA NA
MALALAMIKO HAYO YA MASHABIKI HAO WANAOPIGWA CHENGA KUPEWA UANACHAMA BILA YA
SABABU ZA MSINGI. ISOME..
BARUA YA
WAZI KWA KATIBU MKUU WA COASTAL UNION FOOTBALL CLUB
WAPENZI WA COASTAL FC
P.O.BOX 5152. TANGA.
COASTAL UNION
FC
P.O.BOX 2066,
TANGA.
07.04.2014.
KATIBU MKUU
YAH: MAOMBI
YA KADI ZA UANACHAMA KATIKA CLUB YA MPIRA WA
MIGUU YA COASTAL UNION.
Kichwa cha habari hapo juu kinahusika. Sisi baadhi ya wapenzi
wa coastal union FC ya Tanga. Tumeamua kuandika barua hii kwa katibu mkuu wa
coastal union F na itakuwa ni barua ya
wazi ambayo itaonekana kwenye magazeti na kuzungumzwa katika vyombo vya habari
ili kilio chetu kisikike na wadau wote wa michezo. Pia barua hii tutaipeleka
TFF mkoa wa Tanga na Afisa tamaduni na michezo wa wilaya ya Tanga. Tumeandika
barua hii kwa sababu zifuatazo.
Ukweli ni kwamba hatukuwa na umoja ambao umepanga kuomba kadi
kwa pamoja bali halii hii ya kuungana kwa wapenzi wenye atizo la kutokuwa na
kadi imekuja baada ya wapenzi wa coastal takribani kumi kukutana hapo club wote
wakiwa na nia ya kutaka kupata kadi za uanachama wa coastal.
Lakini kwa bahati
mbaya kila tulipofika hapo club hatukufanikiwa kumpata mtu yeyote anayehusika
na club akiwa katiaka ofisi za club, bali tulipewa mwongozo na fundi nguo
aliyepo hapo nje ya club. Kuwa mkimtaka katibu basi mpigieni simu au kama kuna maagizo
yeyote basi niachieni mimi nitamfikishia. Sisi hatukuridhika kumwachia maagizo
yetu fundi nguo bali tuliamua kumpigia simu marakwamara. Lakin kwa bahati mbaya
simu ya katibu mara nyingi inakuwa haipatikani. Na ikipatika basi haipokelewi.
Baada ya siku mbili tatu za kujaribu kumpigia simu katibu,
mimi mwandishi wa barua hii (Abdullatif
Famau) nilipokea simu kutoka kwa katibu wa coastal union FC. Na maongezi
yalikuwa hivi:
Katibu: hello… nimeona missed call zako
nani mwenzangu?
Abdullatif: mimi naitwa Abdullatif Famau;
nilikupigia simu mara kadhaa baada ya kufika ofisini kwako takribani week mbili
sasa lakini sijakupata, sasa lengo la kukupigia simu niI kutaka kupata card za
uanachama wa timu yetu ya Coastal FC. Na bahati nzuri kuna watu zaidi ya kumi
pia wanataka hizo kadi.
Katibu: sawa Abdul nimekuelewa, lakini
hivi sasa tumesitisha mpango wa kutoa kadi kiholele, kwani tumesikia kuna watu
wamepanga kuja katika timu yetu na kutuletea vurugu. Club ilikuwa mbovu ina
vumbi, haina maji na taa sisi tumetengeneza club tukarudisha maji na Taa, timu
ilikuwa katika low division sisi tukaipandisha mpaka ligu kuu, sasa
hatutakubali waje watu ambao hatuwajui na kutuharibia timu yetu.
AbdulLatif: ooh ok, sasa mwalimu (katibu ni
mwalimu wa shule) watu wenyewe wanaotaka card wote unatufahamu tulichelewa tu
kufuatilia hizo card… labda ni utaratibu gani mbao mmeuandaa ili tuweze kupata
kadi?
Katibu: utaratibu tuliopanga ni kila mtu anayetaka kuwa mwanachama wa
coastal union lazima ajaze fomu maalum na kisha atajadiliwa katika mkutano mkuu
wa wanachama kama awe mwanachama au la..!
Abdullatif: ooh, ok mwalimu. Sasa ni lini
hizo form zitakuwa tayari ili niwaambie jamaa siku ya kuja hapo club?
Katibu: namba yako ninayo, form zikiwa tayari nitakufahamisha. Sawa
Abdul..?
Abdullatif: sawa katibu… ahsante sana..
kwaheri…!
Maongezi
yakaishia hivyo. Na mimi niliwataarifu jamaa wote ambao tulikutana club kwa nia
ya kutaka card.
Tukasubiri zaidi ya
week kupigiwa simu ili kujulishwa utayari wa
fomu. Na pia kila tulipokua tukipata muda tunapita club ili kumjulia
katibu kuhusu fomu lakini kwa bahati mbaya hatukuwahi kumuona katibu akiwa
club.
Sasa tuliamua kuunda umoja wa wapenzi ambao hatuna kadi na
kuhakikisha tunapata kadi kwa haraka iwezekanavyo. Ili tuweze kushiriki mkutano
mkuu wa wanachama ambao utakuwa ni hivi karibuni. Tuliamua tuitane sote ili
tuweze kujadili tufanye nini ili tupate uanachama wa coastal. Kikao chetu cha
mwanzo kilikuwa katika hotel ya splendid viewl. Mnamo tarehe 22 march mwaka huu
saa moja jioni mpaka saa tatu usiku. Agenda kuu ilikuwa nini tutafanya ili
kupata uanachama wa Coastal union fc. Kikao hicho kilihudhuriwa na watu si
chini ya 25, kila mtu alitoa mawazo yake.. laikini mawazo yaliyopita ilikuwa
tumtafute tena katibu ofisini kwake na kumpigia simu na sasa atupe siku maalum
ambayo fomu zitakuwa tayari.
Kweli tulifanya hivyo watu waiimpigia simu siku ya pili yake
na alitoa ahadi kuwa siku ya jumanne ya week ijayo fomu zitakuwa tayari.yaani
tarehe 01.04.2014. Watu wakapeana habari
kwa njia ya simu juu ya ahadi ya katibu, na tulisisitiziana kufika club sote
ambao hatuna card siku hiyo ya jumanne ili kujaza fomu za maombi ya uanachama.
Ilipofika siku ya jumanne. Sio sote tuliofika club lakini
zaidi ya watu kumi walifka club kwa nyakati tofauti na kwa bahati mbaya
hatukufanikiwa kumpata katibu. Kati ya
sisi tulichaguana watu watano ambao wliingiaa kwenye gari yangu ili kwenda
nyumbani kwa katibu baada ya kumpigia simu na ilikuwa haipokelewi na mwisho
ilikuwa haipatikani kabisa. Tuliendesha gari mpaka nyumbani kwake na kwa bahati
mbaya pia hatukumpata lakini tuliacha maagizo kwa mkewe kuwa wapenzi wa coastal
wamefika hapa na wamekuja kwa lengo la kutaka fomu za maombi ya uanachama.
Hivyo ili afahamu ni akina nani wamekwenda nyumbani kwake. Mimi nikaacha jina
langu ili apewe ujumbe.
Baada ya masaa matatu nilipokea ujumbe kwenye simu yangu
kutoka kwa katibu. Na mimi nilimjibu. Mtiririko wa message zetu ulikuwa hivi:
Katibu: nimepata salamu kuwa mmekuja
nyumbani kundi kubwa na familia yangu imetishiwa na ujio wenu. NINAKUKATAZA
KULETA GENGE NYUMBANI, HIYO IWE MWANZO NA MWISHO, AU MTANIONA MMBAYA.kama ni mambo
ya coastal ni club.
Abdullatif: Pole sana mwalimu kwa kukusumbua,
tusamehe kwa kufanya hivyo, ila tumekuwa tukija club kila siku kukuona lakini
hatufanikiwi. Tumesikia kuna watu wamekuja nyumbani kwako na wakapata
waliyoyataka, nasi tukaja huko.
Katibu: wale kadi zao zilikuwa tayari na
wengine majina yao yalikuwepo tangu mwaka jana kwa ajili ya uchaguzi, Nassor
aliwaombea…. Ndio niliowashughulikia….nyie wapya nitakupigia mara tu form zikiwa tayari….
Abdullatif: ok! Ahsante mwalimu. Tutazidi kusubiri
natumai hazitachelewa.
Mwisho wa
majibizano ya ujumbe.
Mpaka leo tunaandika barua hii mheshimiwa Siagi (katibu) hajatufahamisha
kama form ziko tayari. Hivyo basi tuanpenda kujulishwa kwa njia ya maandishi ni
lini form zitakuw tayari.ili na sisi ikifikia kipindi cha mkutano mkuu tuweze
kushiriki na pia kupiga kura ikitokea uchaguzi wa viongozi.
Pia tunapenda kukukumbusha bwana katibu. Utaratibu unaotuekea
sisi wa kujaza fomu na kisha tujadiliwe ndio tuwe wanachama, ndio utaratibu
haswaa ambao katiba ya coastal union inautambua. Rejea katiba ya C.U.F.C TOLEO
LA 2010/2011. KIPENGELE CHA WANACHAMA. IBARA YA 6 na 7 (sifa na utaratibu
wankupata hadhi ya uanachama)
Kitu ambacho kinatushangaza, je wanachama wote waliopo katika
orodha yako wamejaza fomu na kujadiliwa na kupitishwa kuwa wanacha na mkutano
mkuu? Sisi tuna ushahidi ambao unaonyesha wanachama karibia wote hawakujaza
fomu na kama wamejaza basi hawakujadiliwa. Hivyo basi tuna mashaka ya uhalali wao wa uanachama. Na tunathubutu
kusema kutokana na katiba wanachama wengi sio halali bali ni bandia. Na ikiwa
wanachama hao bandia ndio waliotumika
kupiga kura za kuchagua uongozi wa juu ya timu, pia tunahoji uhalali wa
viongozi hao kuwa madarakani.
Kama tulivyotangulia kusema, barua hii itasomeka katika
vyombo vya habari na pia TFF mkoa na AFISA TAMADUNI WA WILAYA. Hivyo tunaomba
kila chombo husika iangalie haki yetu ya sisi kucheleweshwa kupatiwa fomu za maombi
ya uanachama. Na ikionekana uongozi umefanya makosa, basi wawajibishwe ili iwe
mfano kwa timu nyimgine za mpira ambazo zinamilikiwa na wanachama.
Ni matumaini yetu sheria itachukuas mkondo wake kunyamazisha
kilio chetu.
Wako katika michezo
………………………………………………….
Mwakilishi wa wapenzi wa COASTAL UNION FC
ABDULLATIF OMAR FAMAU.
0 COMMENTS:
Post a Comment