Mshambuliaji
mwenye kasi wa Yanga, Mrisho Ngassa amepiga bao tatu au hat trick wakati Yanga
ikishinda kwa mabao 5-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi ya Ligi Kuu Bara
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Ngassa amepiga
bao hizo na alionekana kuwa na kasi zaidi huku akiwapa wakati mgumu mabeki wa
JKT ambayo inapigania roho yake kuepuka kuteremka daraja.
Hussein
Javu na Didier Kavumbagu nao walipiga mabao mengine mawili yaliyoiongezea Yanga
akiba hiyo nzuri ya mabao hadi kufikisha matano.
Bao pekee linalonolewa na Fred Felix Minziro lilifungwa na Nashon Naftali.
Bao pekee linalonolewa na Fred Felix Minziro lilifungwa na Nashon Naftali.
Baada ya
mechi hiyo, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm alisema amefurahishwa na
ushindi huo ambao walistahili kuupata katika mechi zilizopita.
Yanga imepata
ushindi huo bila ya kuwa na mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi pamoja na kipa,
Juma Kaseja ambao hawakuwepo hata kwenye benchi.
0 COMMENTS:
Post a Comment