April 6, 2014


Timu ya Mtibwa Sugar imesisitiza kuwa bado inavutiwa na wachezaji kadhaa akiwemo mshambuliaji wa Simba, Betram Mwombeki.

Mwombeki amekuwa hapewi nafasi ya kutosha kucheza Simba kutokana na Kocha Zdravko Logarusic kuonekana kutovutiwa naye.
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime amesema anaamini Mwombeki ni kati ya wachezaji wazuri.

“Ni kati ya wachezaji wazuri na kama kutakuwa na uwezekano wa kumpata itakuwa vizuri.

“Nia ipo lakini kuna mambo mengi ya kupitia, tuangalie kwanza na sasa nguvu nyingi tunaweka katika mechi zetu za mwisho za msimu.


“Baada ya hapo tutaanza kuangalia tunamhitaji nani na kipi cha kufanya,” alisema Maxime, beki nyota wa zamani wa timu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic