April 30, 2014



Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, ameutaka uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi kusajili wachezaji 25 tu msimu ujao wa ligi kuu ambapo amependekeza kuwa na makipa watatu.

Loga amekabidhi ripoti yake hivi karibuni kabla ya kwenda nchini kwao Croatia kwenye mapumziko huku akisubiri majibu iwapo ataitwa kuendelea na timu hiyo au la ambapo mkataba wake unaisha Juni, mwaka huu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema ripoti hiyo ya kocha aliyoiwakilisha imependekeza kusajili wachezaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukabidhi majina ya wachezaji wanaotakiwa na wasiotakiwa kubaki msimu ujao ambapo idadi kamili anayoitaka ni wachezaji 25.
“Loga amependekeza wachezaji kadhaa wabaki ambao anaona wanafaa kuwatumia kwa ajili ya msimu ujao ambapo amesema anataka wachezaji 25 tu katika timu nzima na iwapo idadi itaongezeka basi itakuwa ni ya viongozi.
“Anahitaji kila nafasi iwe na wachezaji wawili huku kwa upande wa makipa amependekeza waongezwe wawili ili kuwa na jumla ya makipa watatu pamoja na Ivo Mapunda.
“Kuna nafasi mbalimbali ambazo ametaka zisajiliwe, hivyo tutaangalia mahitaji yake iwapo nafasi hizo kuna wachezaji wa Tanzania watakaofaa au kuangalia nje ya nchi kwa kuwa kuna namba nyingine ni lazima tuzipate nje.

“Pia kuna baadhi ya  wachezaji ambao amewapendekeza wasajiliwe kutoka katika timu mbalimbali za ligi kuu, lakini siwezi kuwataja kwa kuwa ni mapema mno,” alisema Kamwaga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic