April 29, 2014


Kamera za uwanjani zimetumika kumnasa yule shabiki aliyetupa ndizi uwanjani akimlenga beki wa Barcelona Dani Alves na Villarreal imetangaza kumfungia maisha kuingia uwanjani hapo.

Shabiki huyo alitupa ndizi wakati Villareal ikipambana na Barcelona lakini Alves akatoa kali ya mwaka kwa kuikota ndizi hiyo na kuila.
Klabu ya Villarreal imetangaza kwamba imemng’amua shabiki huyo kupitia kamera maalum za CCTV kabla ya kutangaza adhabu hiyo kali kabisa.
 Kalbu hiyo imetoa taarifa ifuatayo kuhusiana na shabiki huyo:
"Villarreal CF inapenda kulizungumzia suala hili kwa uwazi, kuwa tumeumizwa sana na jambo hili lililotokea kwenye uwanja wetu wakati wa mechi dhidi ya FC Barcelona baada ya shabiki kutu kwenye Uwanja wa El Madriga ambacho baadaye kiligundulika ni ndizi.
“Kutokana na hali hiyo tumeamua kumpoka tiketi yake ya msimu, lakini tumemuondoa katika mashabiki wanaoruhusiwa kuingia uwanjani katika maisha yake yote na hatatakiwa kugusa El Madrigal.

"Kwa mara nyingine, tunapenda kuweka msisitiza kuwa klabu yetu ni mfuasi wa michezo kwa wote na usawa, haki, heshima ndani na nje ya uwanja.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic