Timu ya Taifa ya Malawi (Flames)
inatarajiwa kuwasili nchini Mei 1 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki
dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Mei 4 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine jijini Mbeya.
Flames yenye msafara wa 31
utakaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu cha
Malawi (FAM) utaingia Mbeya kwa usafiri wa barabara. Wachezaji katika msafara
huo ni 20.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha mpya, Mart Nooij tayari ipo
jijini Mbeya kujiwinda kwa mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya
mashindano dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16
na 18 mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment