Atlético de Madrid watatua jijini Lisbon, Ureno
siku moja tu kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.
Kikosi hicho cha Diego Simeone kimekuwa na kawaida ya kutua siku moja tu
kabla ya mechi hasa inapokuwa katika michuano ya kimataifa.
Kwa mujibu wa ratiba yao, baada ya kutua Atletico watafanya mazoezi siku
hiyo wlaiyofika na baadhi ya wachezaji watakwenda kuzungumza na waandishi wa
habari.
Baada ya hapo watapumzika siku hiyo jioni na siku iliyofuata watapiga
fainali na siku moja baada ya fainali wataondoka kurejea Madrid.
Kwa kifupi, tayari Kombe litakwenda katika jiji la Madrid nchini Hispania. Lakini
haijulikani nani atarudi nalo kutoka Lisbon.
0 COMMENTS:
Post a Comment