Mshambuliaji Lionel Messi wa Barcelona ameiomba klabu yake kumsaini nyota wa
Manchester City, Kun Aguero.
Kupitia baba yake ambaye ni meneja wake, Messi ameonyesha nia yake ya kuona
Aguero ambaye ni raia mwenzake wa Argentina akisainiwa na timu yake.
Baba yake, Jorge Messi, alikutana na mmoja wa Wakurugenzi wa Barcelona, Javier
Faus na kumueleza kuhusiana na suala
hilo laini pia Messi anaamini ni wakati wa kumuongezea mkataba kipa Pinto.
Kwa mujibu runinga ya Catalan 'TV3', imeeleza kuwa Messi yuko tayari kubaki
Barcelona, lakini anaamini Aguero atakuwa msaada mkubwa.
Aguero ana uwezo mkubwa na amekuwa msaada kwa man City ambayo ina nafasi
kubwa ya kutwaa ubingwa wa England, ila tatizo lake kubwa ni kuwa majeruhi mara
kwa mara.
Messi na Aguero wamekuwa marafiki wakubwa tokea wakiwa katika timu ya vijana ya Argentina.
0 COMMENTS:
Post a Comment