MBELWA AKIJARIBU KUTEREMKA ULINGONI ILI KUMFUATA NYILAWILA WAZICHAPE KAVUKAVU. |
Vyama vya
ngumi za kulipwa Tanzania vimekutana na kwa pamoja kukubaliana kumfungia bondia
Said Mbelwa kwa miezi sita.
Mbelwa
alianzisha fujo na kutoka nje ya ulingo na kutaka kuzichapa na Karama
Nyilawila.
Katika
pambano hilo kuwania ubingwa wa UBO kwenye Ukumbi wa Friends Corner, Manzese
jiji Dar es Salaam.
Pambano hilo
lilivunjika Nyilawila akiwa anaongoza, Mbelwa akadai alipigwa kichwa.
Lakini
baadaye Nyilawila naye alipigwa chupa na shabiki aliyedaiwa kuwa wa Mbelwa.
Pia mabondia
maarufu Mada Maugo na Thomas Mashali ambao walikuwa watazamaji walizichapa
kavukavu.
Katibu Mkuu
wa PST, Anthony Rutta amethibitisha kusimamishwa kwa Mbelwa kwa miezi sita
kuanzia wiki iliyopita siku aliyofanya vurugu.
0 COMMENTS:
Post a Comment