WAMBURA |
Mgombea wa
urais katika klabu ya Simba aliyeondolewa kugombea na kamati ya uchaguzi ya
klabu hiyo, atakata rufaa.
Michael
Richard Wambura ameondolewa kushiriki uchaguzi kwa kuwa si mwanachama.
Kwa mujibu
wa kamati hiyo, Wambura alisimamishwa uanachama kutokana na kitendo chake cha
kuipeleka Simba mahakamani, lakini hakuwahi kurudishwa.
Lakini
Meneja wa kampeni wa Wambura, Majaliwa Mbasa amesema watakata rufaa.
“Tutakata
rufaa TFF kupitia kamati ya rufaa na tunaamini Wambura atapata haki yake
agombee.
“Sisi
tunaona si sawasawa kabisa, hivyo hatuwezi kuacha hili suala lipite tu,”
alisema Mbasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment