Taifa Stars
imeishinda Malawi kwa bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa leo kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la
mechi hiyo lilifungwa na Amri Kiemba dakika ya 36 baada ya pasi nzuri ya
Shomari Kapombe.
Stars
ilicheza vizuri zaidi katika kipindi cha pili baada ya kocha Mart Nooij kufanya
mabadiliko na kuingiza wachezaji wakongwe.
Stars
itaondoka kesho kwenda Harare, Zimbabwe kuwavaa wenyeji kwa ajili ya mechi ya
marudiano kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Katika mechi
ya kwanza, Stars ilishinda kwa bao 1-0 jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment