Wanachama wa Simba kupitia Tawi la Ubungo Terminal la jijini Dar es Salaam, wapo katika
mchakato kabambe wa kuwachambua kimyakimya wagombea wa nafasi ya makamu wa rais
wa klabu hiyo ili waweze kumpata mmoja watakayemuunga mkono kama ilivyo kwa
mgombea wa kiti cha urais, Evans Aveva.
Mwenyekiti wa Tawi la Ubongo Terminal, Justin Joel,
alisema hali hiyo inawapa wakati mgumu kwa sasa lakini baada ya muda watapata
jibu juu ya suala hilo.
Alisema
hivi sasa wapo katika mchakato wa kuwachambua wagombea hao kimyakimya bila ya
wao kujua na mwisho wa siku watampata mmoja watakayemuunga mkono mwanzo mwisho
katika uchaguzi huo.
“Nkwabi na
Kaburu kila mmoja ana upungufu wake lakini kwa hivi karibuni, tutajua tu kuwa
tumuunge nani katika mchakato huo kwani tunataka mtu wa kutuletea mafanikio,”
alisema Joel.
0 COMMENTS:
Post a Comment