Mgombea wa kwanza kuchukua fomu ya kwanza
ya kugombea nafasi ya urais katika klabu ya Simba amekuwa Evans Aveva.
Aveva ameweka rekodi ya kuwa wa kwanza
kuchukua fomu hiyo, lakini ameweka rekodi ya kusindikizwa na watu wengi zaidi.
Aveva amechukua fomu hiyo kwenye makao
makuu ya klabu ya Simba, barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam huku
akisindikizwa na kundi kubwa la wanachama na mashabiki wa Simba.
Maandamano ya kumpeleka Msimbazi yalianzia
katikati ya jiji la Dar hadi Kariakoo huku Aveva akiwa kwenye gari la wazi.
\Aveva ambaye amekuwa Simba kwa zaidi ya
miaka 20, huk akiongoza kamati kadhaa ikiwemo ya usajili alionyesha ni mwenye
fuaha sana.
“Nashukuru sana, nimechukua fomu kwa kuwa
ni haki yangu, lakini nataka kuitumikia Simba na mapokezi huku wanachama na
mashabiki wakinisindikiza kwa wingi imenipa nguvu.
“Sitapenda niseme mengi lakini matarajio
yangu ni kufanya vizuri kwenye uchaguzi na pia kupambana kuleta mabadiliko
Simba,” alisema.
Aveva ndiye aneyepewa nafasi kubwa zaidi
ingawa haijajulikana nani mwingine atachukua nafasi hiyo.
Hata hivyo wanachama waliokuwa
wameandamana walionyesha kutaka uchaguzi ufike haraka.
“Uchaguzi ni Juni 29, ila tunatamani ufike
leo, tunataka kumpa nafasi Aveva, kweli tumechoka kunyanyaswa.
“Simba leo hatuna tofauti na JKT, uongozi
uliokuwepo umetuumiza vya kutosha. Tumevumilia sana, sasa acha tumpe Aveva,”
alisema mmoja wanachama waliokuwa kwenye pikipiki akijitambulisha kwa jina la
Said.
subirini tuone kama atakuwa chaguo sahihi
ReplyDelete