Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf
Manji amesema kuondoka kwa wachezaji wao wawili Didier Kavumbagu na Frank
Domayo sio mwisho wa timu ya Yanga, kwani uongozi wake unaendelea na mipango ya
kuhakikisha inasajli wachezaji wengine wazuri ambao wataisadia timu kwenye
msimu ujao kwa kufuata maelekezo ya Benchi la Ufundi.
Akizungumza na waandishi wa habari makao
makuu ya klabu leo, Manji amesema yameongelewa mengi sana kwa kipindi cha mwezi
mmoja ambao hakuwepo nchini kwa ajili ya kazi zake binafsi lakini sasa amerejea
na maandalizi ya msimu ujao yameshaanza.
Kuondoka kwa Kavumbagu ni kutokana na
kuchelewa kwa majibu ya TFF juu ya idadi ya wachezaji wageni kwa msimu mpya,
huku Domayo ambae tangu mwaka jana aliombwa kuongeza mkataba alikua akisema
anamsubiria mjomba wake ndipo aweze kufanya hivyo.
Pamoja na kuondoka kwa wachezaji hao bado
kwa kushirikiana na kocha Hans watahakikisha Yanga inaendelea kutisha msimu
ujao na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, Hans aliahidi kuleta
wachezaji wazuri watakaoisaidia Yanga siku alipokua akiiongea na waandishi wa
habari kuwaaga.
Aidha, Manji amelifuta rasmi tawi la
Tandale kutokana na kuwa na chanzo cha vurugu na migogoro ndani ya klabu, pia
amewafuta uanachama wanachama sita ambao walikiuka katiba ya Yanga kwa kwenda
kuongea na waandishi na HABARI bila ya Idhini ya uongozi huku pia wakishindwa
kulipia ada zao za uanachama kwa zaidi ya miezi sita, waliofutwa uanachama
ni:
1. Ally Kamtande, 2. Isiaka Dude, 3.
Hamisi Matandula, 4.Waziri Jitu Ramadhani, 5.Mohamed Kigali Ndimba , 6. Selaman
Hassan Migali
Mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba
utafanyika terehe mosi Juni, 2014 katika Ukumbi wa Oysterbay Police Mess na
wanachama wote wanaombwa kulipia ada zao ili waweze kuhuhudhira mkutano huo
wakiwa hai.
Suala la ujenzi wa Uwanja wa Kisasa eneo
la Jangwani bado lipo pale pale, kikubwa kinachosubirwa ni majibu ya serikali
juu ya maombi ya eneo la ziada, kwani Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alisema
suala hilo lipo ukingoni na mda si mrefu.
haya tumekusikia
ReplyDelete