AVEVA (KUSHOTO) AKIWA NA BAADHI YA WADAU, BENNY KISAKA NA JUMA PINTO AMBAYE NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TANZANIA (TASWA). |
Mmoja wa watakaowania nafasi ya Rais mpya wa klabu ya Simba, Evans Aveva atachukua fomu kesho.
Taarifa zinasema Aveva ataongozana na
rafiki zake kadhaa ambao watamsindikiza katika makao makuu ya Simba kuchukua
fomu hizo.
Aveva ni kati ya wanachama wa Simba
wanaounda kundi la Friends of Simba na amewahi kuliongoza kwa mafanikio.
Ni kati ya wanaopewa nafasi kubwa kuitwaa
nafasi hiyo baada ya Zacharia Hans Pope kukosa nafasi ya kushiriki.
0 COMMENTS:
Post a Comment