Huku klabu kongwe za Simba na Yanga zikiendelea
kushangaa-shangaa, Mbeya City yenyewe inatarajia kuanza ujenzi wa uwanja wake
eneo la Iwambi Julai, mwaka huu.
Timu hiyo mpya kabisa inayomilikiwa na Manispaa ya Jiji la Mbeya, inaonekana
kuwa na mikakati kabambe baada ya kuushangaza umma kwa kumaliza katika nafasi
ya tatu katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara.
Katibu wa timu hiyo, Emmanuel
Kimbe, alisema huenda ujenzi huo ukaanza katika mwaka mpya wa fedha wa Julai.
Alisema wanafanya hivyo ili kuweza kuwa na uwanja wa mazoezi kwa
sababu uwanja huo utajengwa katika awamu tatu kama walivyokuwa wameainisha
awali.
“Ujenzi wa uwanja wetu mpya utaanza katika mwaka mpya wa fedha
ujao. Matarajio yetu yetu ni kwamba, kuanzia Julai, mwaka huu ndiyo tutaanza
kazi hiyo ya ujenzi.
“Na uwanja utajengwa katika awamu tatu kama tulivyokuwa tumepanga
mwanzo, mafanikio yatakayojitokeza mwanzo ndiyo yatatufanya tusonge mbele
zaidi,” alisema Kimbe.
0 COMMENTS:
Post a Comment