Kocha Mkuu
wa Uganda ‘The Cranes’, Sredojevic Milutin ‘Micho’ amesema bao pekee la Hamisi
Kiiza ndiyo limewaweka kwenye matumaini ya kuwang’oa Madagascar.
The Cranes
walipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Madagascar katika mechi ya
kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Mataifa Afrika.
Kiiza ndiye
alifunga bao pekee la Uganda katika hatua za mwisho wakati Uganda ikiwa nyuma kwa
mabao 2-0.
Ushindi wa
bao 1-0 tu mjini Kampala utawapa nafasi Uganda ingawa Micho ambaye ni kocha wa
zamani wa Yanga, amesema wanataka kushinda kwa mabao mengi.
“Hata ikiwa
tatu au nne, itakuwa ni jambo la msingi lakini tayari ni mechi ngumu.
“Bao moja
la Kiiza linatuvuta kwenye njia nzuri ya mapambano kwa kuwa tunataka kuvuka,”
alisema micho raia wa Serbia.
0 COMMENTS:
Post a Comment