Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClemen amewasili nchini leo alfajiri (Mei 4 mwaka
huu) ambapo atakuwepo kwa siku tatu.
McClemen ameondoka leo (Mei 4 mwak huu) kwenda Bukoba ambapo
atakagua Uwanja wa Kaitaba, na kesho (Mei 5 mwaka huu) atakwenda jijini Mwanza
kukagua Uwanja wa Nyamagana.
Viwanja hivyo vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA
chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClemen
atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa
kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa
kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume
(Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
0 COMMENTS:
Post a Comment