Mshambuliaji wa Simba, Betram Mwombeki, amesema
anaamini ataendelea kubaki kwenye timu hiyo licha kutocheza mechi nyingi msimu
ulioisha mwezi uliopita.
Mwombeki amesema anachokifanya katika
kipindi hiki ni kuangalia mpangilio wa timu jinsi utakavyokuwa kutokana na kuwa
bado ana mkataba wa kuitumikia timu hiyo.
“Nitaangalia mpangilio wa timu kama
nikiridhika nao basi nitaendelea kuwepo kwa sababu hata mzunguko wa pili
sikufanya vizuri kutokana na kuumwa lakini bado nina mkataba nao wa mwaka
mmoja.
“Hata kama Loga akirudi kwenye timu,
kwa upande wangu nitakuwa tayari kuendelea kufanya naye kazi na kujituma
mazoezini na baadaye aweze kuniamini,” alisema Mwombeki ambaye kuna wakati
ilibidi afarijiwe na wachezaji wenzake baada ya Loga kumuingiza uwanjani kisha
kumtoa baada ya dakika tano tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment