May 8, 2014



Sundeland imeipiga Wes Brom kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu England, iliyomalizika hivi punde.

Kutokana na ushindi huo, Sunderland imefikisha pointi 38 na kuepuka kuteremka daraja.

Mabao ya Sunderland yalifungwa na Jack Colback katika dakika ya 13 na Fabio Borin kwenye dakika ya 31.
Hata kama itapoteza mechi ya mwisho na kubaki na pointi 38, Norwich yenye 33, ikashinda bado itakuwa na 36.
Kubaki kwa Sunderland, maana yake rasmi Norwich imeungana na Fulham na Cardiff kuiaga Premiership na kurejea Ligi Daraja la Kwanza England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic