Man City wamemla ng’ombe mzima na sasa
wamemaliza mkia tu.
Ushindi wao wa mabao 4-0 dhidi ya Aston
Villa, maana yake wanatakiwa kushinda mechi yao ya mwisho dhidi ya West Ham
United wakiwa nyumbani Etihad na kubeba kombe la Ligi Kuu Englan.
Ushindi wa leo wamefikisha pointi 83
wakifuatiwa na Liverpool wenye 81.
Liverpool ndiyo timu nyingine yenye nafasi ya
kutwaa ubingwa kama itashinda mechi ya mwisho dhidi ya Newcastle na City
wapoteze dhidi ya West Ham.
0 COMMENTS:
Post a Comment