Beki kiraka wa
kimataifa wa Yanga, Mbuyu Twite ameitaja timu yake kuwa ndiyo iliyoweka kizuizi
cha yeye kujiunga na Lupopo FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Kongo.
Twite ambaye mkataba
wake wa kuichezea Yanga ulimalizika Aprili 19, mwaka huu alikuwa mbioni kuondoka
klabuni hapo lakini mambo yakawa yanaenda ndivyo sivyo.
Twite amesema kuwa alipanga kurejea kwao mapema kwa ajili ya
kufanya mazoezi kwenye kikosi cha Lupopo lakini imekuwa ngumu.
“Nilipanga kurejea
nyumbani mapema mara baada ya ligi kumalizika, lakini imeshindikana kutokana na
Yanga kunizuia hadi tutakapomalizana katika usajili wangu kwa ajili ya msimu
ujao.
“Kama unavyojua ni
ngumu kwa mchezaji kukaa muda mrefu bila kufanya mazoezi katika kipindi hiki
ambacho ligi imesimama kwa hofu ya uzito kuongezeka.
“Nyumbani ligi
inaendelea, timu shiriki zinajiandaa, hivyo nilipanga kurudi haraka kwa ajili
ya kufanya mazoezi na Lupopo, lakini imeshindikana, hivyo nitajiunga nayo baada
ya kumalizana na viongozi wa Yanga,” alisema Twite.
0 COMMENTS:
Post a Comment