LUIZIO AKIWA NA UZI WA AMAZULU WAKATI WA MAJARIBIO NCHINI AFRIKA KUSINI (PICHA KWA HISANI YA ABRAHAM RICE) |
Mshambuliaji wa Mtibwa
Sugar Juma Luizio amefanya majaribio katika timu ya Amazulu inayoshiriki Ligi
Kuu Afrika Kusini na
kuwavutia benchi la ufundi la timu hiyo.
Luizio alifanyiwa ‘mchongo’
huo na Mtanzania anayeishi jijini Mwanza anayeitwa Jacob Kabole.
“Huyo ndiye kawafanyia
mpango na Luizio amefanya vema katika majaribio ya hapa Amazulu,” kilieleza
chanzo cha habari kutoka Afrika Kusini.
“Pamoja na Luizio
kulikuwa na kijana anaitwa Kheri Mohamed Khalifa anayechezea Toto
Africans na wote wamefanya vema, majibu yanasubiriwa.
“Baada ya Amazulu
walipelekwa Martzburg ambayo walifanya siku tano tu, hawakumaliza likaingia
suala la ligi, hivyo wameambiwa warejee baada ya Kombe la Dunia kumalizia
majaribio.”
Alipotafutwa Luizio
jana, alisema: “Niko katika sehemu ambayo siwezi kuzungumza.”
Gazeti hili likafanya
juhudi ya kumtafuta Kabole ambaye pia alisema yuko kwenye kikao asingeweza
kuzungumza.
Luizio ni kati ya
wachezaji waliounda kikosi cha Young Taifa Stars ambacho kwa mara ya kwanza
kiliteuliwa na kocha Kim Poulsen.
0 COMMENTS:
Post a Comment