June 28, 2014



Brazil imevuka hadi robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuitoa Chile kwa mikwaju ya penalti 3-2.
Timu hizo zililazimika kuingia katika mikwaju ya penalti baada ya kuvuka dakika 120 ya hatua ya 16 Bora zikiwa sare ya bao 1-1.
William na Hulk ndiyo waliokosa penalti mbili za Brazil na Alexis na Jara wakakosa za Chile huku kipa wa Brazil, Julio Cesar mwenye miaka 34 akiwa shujaa kwa kupangua penalti mbili ikiwemo ya Sanchis.


Brazil ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 18 kupitia kwa David Luiz anayekipiga Chelsea.
Lakini Chile wakasawazisha katika dakika ya 32 kwa shuti la kimo cha panya kupitia kwa Alexis Sanchez anayekipiga Barcelona.


Alexis alifunga bao hilo baada ya uzembe wa mabeki wa Brazil kumpa nafasi ya kupiga shuti hilo kiufundi.
Baada ya hapo, mechi ilizidi kuwa ngumu huku kila upande ukikosakosa.
Brazil ndiyo walipata nafasi kadhaa safi zikiwemo zile kupitia Fred, Jo na Hulk lakini kutolenga lango, kuzubaa au umahiri wa kipa wa Chile, kuliikosesha bao Brazil.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic