June 28, 2014

AVEVA..


Mgombea wa urais wa Simba, Evans Elieza Aveva ambaye anapewa nafasi kubwa kutwaa kiti hicho ameamua kuvunja makundi yote, siku moja tu kabla ya uchaguzi.

Uchaguzi mkuu wa Simba unafanyika kesho kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi Osyterbay jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kupewa nafasi ya kuchukua urais wa Simba kwa mara ya kwanza, Aveva ametangaza kuvunja makundi na kutaka Simba moja.

Aveva ameyasema hay oleo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

“Simba inataka umoja kweli, utaona leo nimeamua kuwakaribisha wagombea wote kufanya kampeni za mwisho na mimi.

“Sikujali suala la itikadi wala chochote, najua Simba inahitaji umoja, nataka tuungane na kutengeneza Simba moja imara.

“Tufanye uchaguzi lakini lazima tujue lengo la Simba ni maendeleo na mafanikio hayawezi kupatikana kama hakuna umoja,” alisema Aveva.

Aveva anayejulikana kwa mipango ya usajili, pia alisema atahakikisha Simba inafanya kazi kubwa ya kusajili wachezaji sahihi.
Alisema Simba haitasajili wachezaji waliochoka na badala yake wale watakaifanya irudi katika heshima yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic