June 29, 2014



Evans Elieza Aveva amefanikiwa kumshinda mpinzani wake Andrew Tupa na kuweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza wa Simba Sports Club wa ngazi ya juu kuliko zote kutumia jina la Rais.
Pia mashabiki wa Geofrey Nyange 'Kaburu' aliyekuwa anagombea makamu wa rais nao wameanza kushangilia wakionyesha wamepata matokeo kwamba amewashinda akina Sued Nkwabi na Jamhuri Kiwhelo 'Julio'.

Aveva amemshinda Tupa kwa idadi kubwa ya kura katika uchaguzi uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya Aveva kutangazwa mshindi, cheleko kutoka kwa wafuasi wake zilianza.
TAARIFA ZAIDI KUHUSIANA NA IDADI YA KURA NA WAGOMBEA WENGINE ZINAFUATIA.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic