June 29, 2014

WAGOMBEA WA KITI CHA URAIS SIMBA, ANDREW TUPA (KUSHOTO) NA EVANS AVEVA WAKISUBIRI MATOKEO WAKATI KURA ZIKIHESABIWA.


Baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika, kazi ya kuanza kuzihesabu kwenye uchaguzi wa Simba zimeanza.
Uchaguzi huo unafanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Zoezi la upigaji kura limekwenda vizuri na sasa katika eneo hili minong'ono ndiyo imechukua nafasi kubwa.

Kila anayezungumza anaamini fulani huenda akachukua nafsi fulani lakini wagombea wamejituliza kimya wakisubiri majibu.

Huenda zoezi hilo likachukua takribani saa mbili kabla ya kazi ya kutangaza wagombe kufanywa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic