June 29, 2014



Mgombea wa kiti cha makamu wa rais wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya wanachama wa klabu hiyo kumzomea.
Uchaguzi huo unaendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.


Tukio hilo limetokea wakati Julio akijieleza kwa nini apewe nafasi hiyo, lakini yeye akataka kuwataja baadhi ya watu kama ni tatizo, wanachama wakamzomea.
Kuona hivyo, Julio alikuwa mwepesi, hivyo hakuendelea kuzungumza na baadaye akaendelea kufafanua mambo mengine.
Baadye Julio aligeuka shujaa baada ya wanachama hao kumshangilia tena kutokana nay eye kujibu kwa ufasaha swali aliloulizwa na wanachama.
Kwanza Julio alitoa kali, aliamua kujiuliza mwenyewe kumsahihisha yule mwanachama halafu akajibu pia kwa ufasaha.
Kutokana na hali hiyo, wanachama hao walimshangilia kwa nguvu na kufanya nafasi ya makamu wa rais kuzidi kuwa ngumu.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic