June 30, 2014




Kwa mara ya kwanza, Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maxim oleo amekutana na wachezaji wa Yanga.


Maximo ameanza kazi rasmi leo kwa kuzungumza na baadhi ya wachezaji wa Yanga katika mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu hiyo leo.

Katika mkutano huo Maximo aliwaeleza mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kusisitiza umuhimu wao kuhusiana na mafanikio ya klabu hiyo.
Baada ya mkutano huo wa leo, Yanga watakuwa tayari kuanza mazoezi chini ya Mbrazil huyo aliyewahi kuinoa Taifa Stars.
Mkutao huo umehusisha wachezaji ambao hawako kwenye vikosi vya timu ya taifa pamoja na benchi la ufundi.
Pia baadhi ya viongozi watendaji wa Yanga walihudhuria kikao hicho kilichoanza saa 3 kamili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic