Michael
Wambura amelifikisha suala lake na mwanasheria mkongwe nchini Dokta Damas
Daniel Ndumbaro kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Wambura
amelifikisha suala hilo kwenye kamati ya maadili ya TFF baada ya Ndumbaro kufunguka
Jumapili iliyopita.
Ndumbaro ambaye
ni mwenyekiti wa kamati ya uchaghuzi ya Simba alieleza mambo kadhaa akijibu
mapigo ya Wambura ambaye awali alitangaza kumchangishia fedha ili aende
akasome.
Lakini
Ndumbaro akasema ameishamaliza madarasa yote na kumtaka Wambura achangishe
fedha kwa ajili ya kujilipia ada kwa kuwa inamshinda.
Pia Ndumbaro
akasema yeye ni mwalimu wa Wambura katika Chuo Kikuu Huria (Out) na anaujua
udhaifu wake ingawa maadili yanamzuia kuutangaza hadharani.
Wambura
amesema Ndumbaro alimshambulia nje ya masuala ya uchaguzi, hivyo anataka kamati
hiyo ya maadili ya TFF ichukua hatua.
Sakata hilo
lilianza baada ya kamati ya uchaguzi ya Simba chini ya Ndumbaro kumuengua
Wambura na kutangaza kuwa alisimamishwa uanachama.
0 COMMENTS:
Post a Comment