Wachezaji
wawili waliochaguliwa kwenda kwenye kambi ya Copa Coca-Cola ya Dunia nchini
Brazil wamekabidhiwa bendera tayari kwa safari hiyo inayofanyika leo (Juni 4
mwaka huu).
Hafla
ya kukabidhi bendera hiyo kwa Ali Shabani Mabuyu na Juma Yusuf imefanyika leo
katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Naibu Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Juliana Yassoda ndiye alikabidhi bendera.
Wakati
Mabuyu kutoka Ilala alikuwa mchezaji bora wa michuano ya Copa Coca-Cola kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 15 kwa mwaka 2013/2014, Yusuf kutoka Zanzibar
ndiye aliyeibuka mfungaji bora katika michuano hiyo.
Wachezaji hao watakuwa katika kambi hiyo
itakayokuwa katika Jiji la Sao Paulo kwa siku kumi ambapo watafundishwa masuala
mbalimbali ya mpira wa miguu. Pia watashuhudia mechi ya ufunguzi ya Fainali za
Kombe la Dunia katika ya wenyeji Brazil na Croatia itakayochezwa Juni 12 mwaka
huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment