July 12, 2014



Familia ya Coastal Union inazidi kumeguka baada na mmoja wa wanachama na wakurugenzi kuamua kuhamia katika klabu ya African Sports.

African Sports maarufu kama Wana Kimanumanu ni wapinzani wakubwa wa Coastal Union na sasa wamepanda daraja hadi la kwanza.

Mohamed Ahmed Bin Slum ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Bin Slum Tyres ameamua kuhamia African Sports kutokana na kuona hakuna aliyekuwa akidhamini mchango wa familia yake kupitia kampuni ya Bin Slum iliyotumia zaidi ya Sh milioni 300 kwa ajili ya kuisaidia Coastal Union.

“Vizuri kufanya kazi na watu wanaodhamini mchango wako, hata kama utakuwa unatoa kidogo,” alisema Bin Slum.

Viongozi wa Coastal Union wamekuwa kwenye mgogoro na kampuni ya Bin Slum ambayo ilifanya makubwa kuisaidia timu hiyo tokea inapambana kurejea ligi kuu.
Lakini jana kulikuwa na taarifa za Mwenyekiti wake Ahmed Aurora kuachia ngazi ingawa yeye hakupatikana kuthibitisha hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic