July 12, 2014



Wakati Yanga ikiwa imeamua kumtafutia nyumba kocha wake, Marcio Maximo, milionea Zacharia Hans Poppe ameamua kutoa moja ya mijengo anayoimiliki kwa ajili ya Kocha, Zdravko Logarusic.


Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba, Hans Poppe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, ametoa nyumba hiyo iliyo uzunguni Kunduchi Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mtoa habari amesema nyumba hiyo ya kisasa, kama itapangishwa kodi yake ni dola 2,000 na kuonyesha amepania kufanya kweli, amenunua samani zinazoelezwa kufikia zaidi ya Sh milioni 10 kwa ajili ya matumizi ya kocha huyo.

“Kila kitu kimefanyika, makochi ya kisasa na vitu vingine vimeingia ndani ya nyumba na leo kuna watu walimchukua kocha na kumpeleka Kunduchi. Pia unaweza kupitia kule Boko Ununio halafu ukatokea kwa kocha,” kilieleza chanzo.

Awali, Loga raia wa Croatia alikuwa akiishi katika moja ya hoteli katikati ya jiji la Dar es Salaam. Aliishi hapo nusu msimu alioifundisha Simba, kabla ya kwenda kwao kwa mapumziko.

Pamoja na nyumba hiyo, imeelezwa milionea huyo yuko safari lakini akirejea, Loga atakabidhiwa  gari la kisasa na litakuwa ni 4 Wheel, kwani Maximo pia anatumia Toyota Prado, ambalo ni 4 Wheel pia.

Tayari Loga ameingia kwenye nyumba hiyo na kukabidhiwa ufunguo wa nyumba na kumaliza maombi yake kuwa anahitaji nyumba nzuri ya kuishi badala ya kuishi hotelini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic