July 10, 2014



Shirikisho la Soka la KImataifa (Fifa), imeifungia Nigeria kushiriki michuano ya kimataifa.
Fifa imeifungia Nigeria kwa muda usiojulikana kutokna na serikali kuliingilia shirikisho la soka la nchi hiyo NFA.
Maana yake Nigeria pamoja na klabu zake zote za soka Nigeria hazitashiriki michuano ya kimataifa.

Fifa imeamua kuchukua uamuzi huo baada ya serikali ya Nigeria kuusimamisha uongozi wa NFA kwa madai kwamba ulifanya madudu wakati timu ya taifa ya nchi hiyo ikishiriki Kombe la Dunia.

Lakini Fifa ikaonya kwamba si sahihi kuingilia masuala ya soka, serikali ya Nigeria haikutekeleza onyo hilo la Fifa kwa kulisikiliza na kulifanyia kazi. Mwisho shirikisho hilo limepitisha uamuzi wa kuifungia Nigeria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic