Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Lina Kessy
ameteuliwa kuwa Ofisa Michezo wa Umoja wa Afrika (AU).
Uteuzi huo
umefanywa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Nkozasana Dlamini-Zuma, na Lina
atatumikia nafasi hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu katika makao makuu ya AU
yaliyopo Addis Ababa, Ethiopia.
Lina ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) amewashukuru
wote ambao kwa michango yao ya hali na mali imemwezesha kufika hapo.
Ameishukuru TFF
kwa kumlea na kumjenga. Shukrani nyingine amezitoa kwa Serikali kupitia
Kurugenzi ya Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya Olimpiki
Tanzania (TOC).
TFF inampongeza kwa uteuzi huo, na tunaamini
ataipeperusha vyema bendera ya Tanzania ikiwemo kuwa chachu ya maendeleo ya
michezo kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
0 COMMENTS:
Post a Comment