Timu ya Taifa ya
Msumbiji (Mambas) inawasili Dar es Salaam kesho (Julai 18 mwaka huu) kwa ajili
ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili,
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mambas itatua
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7.30 mchana kwa ndege
ya LAM ikiwa na msafara wa watu 37 ambapo kati ya hao, 25 ni wachezaji.
Wachezaji kwenye
msafara huo ni Almiro Lobo, Apson Manjate, Bone Mario Uaferro, Dario Ivan Khan,
Edson Sitoe, Eduardo Jumisse, Gelicio Aurelio Banze, Helder Pelembe, Josemar
Machaisse, Elias Pelembe, Isac Carvalho na Jeffrey Constatino.
Wengine ni Manuel
Fernandes, Manuel Uetimane, Mario Sinamunda, Momed Hagi, Reginaldo Fait,
Reinoldo Mandava, Ricardo Campos, Saddan Guambe, Simao Mate Junior, Soares
Victor Soares, Stelio Ernesto, Vando Justino na Zainadine Junior.
Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya Accomondia, na
itaondoka Jumapili mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na
mwamuzi Mahmoud Ashour.
0 COMMENTS:
Post a Comment