SALEH AL RAWAH AKIPAMBANA UWANJANI KATIKA SHULE YA MAFUNZO CHINI YA REAL MADRID. |
Yule kinda
mtoto wa kigogo wa Simba aliyewahi kuandikwa na gazeti hili wakati akikipiga
Arsenal tawi la Oman, sasa ametua Real Madrid.
SALEH AL RAWAH AKIFAYA VITU MBELE YA WENZAKE |
Saleh amekuwa
kivutio kutokana na uwezo wake mkubwa licha ya umbo lake kuonekana ni dogo
ukilinganisha na wenzake.
MUSLEY |
Wakati
akicheza kwenye shule ya watoto ya Arsenal jijini Muscat, Saleh alilazimika
kurushwa na kucheza na wale wanaomzidi umri zaidi ya miaka mitano.
Baba yake
amethibitisha taarifa hizo zilizowekwa kwenye mtandao wa Shirikisho la Soka
Oman (Ofa) kuwa amekuwa kivutio kwa timu kubwa.
“Ni kweli
Saleh amepata nafasi hiyo ya Real Madrid, lakini ni suala la familia sasa na
tunapaswa kulijadili.
Naomba niachie kwanza nilifanyie kazi nitakupa taarifa
baada ya kufika Oman,” alisema Al Rawah.
Kinda
huyo amekuwa akifananishwa na Lionel Messi kutokana na kasi yake uwanjani
lakini uwezo mkubwa wa kuwapiga chenga wakiwemo wale wanaomzidi umri.
Kawaida klabu kubwa kama Arsenal, Real
Madrid na nyinginezo zimekuwa na shule maalum za watoto katika nchi mbalimbali
barani Asia ikiwemo Oman.
0 COMMENTS:
Post a Comment