July 11, 2014



Pamoja na Juan Zuniga wa Colombia kumpigia simu na kumuomba msamaha Neymar kutokana na kumuumiza, bado mshambuliaji huyo wa Brazil alimwaga soka chozi wakati akielezea kwamba ilibaki kidogo apooze.

Neymar, alizungumza kwa mara ya kwanza tokea aumie katika mechi ya robo fainali dhidi ya Colombia na kulazimika kukimbizwa hospitali.
Huku akimwaga machozi mbele ya waandishi wa habari alisema aliumia sana baada ya kupewa taarifa kwamba ilibaki muda mchache kabla ya kupooza.
Pia, Neymar alimtetea kocha wake, Luiz Felipe Scolari kwamba si mzee kama ambavyo wamekuwa wakisema watu baada ya Brazil kuchapwa mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani na kusisitiza ni kati ya makocha bora duniani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic