July 11, 2014

SIKU BIN SLUM WALIPOINGIA MKATABA NA BIN SLUM KUPITIA TAIRI ZAKE ZA DOUBLE STAR


Timu ya Stand United ya Shinyanga ipo katika harakati za kumsajili straika raia wa Burundi kwa ajili ya msimu ujao.
 Timu hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Bin Slum Tyres Ltd kupitia tairi zake aina ya Double Star inaonyesha imepania kufanya makubwa msimu ujao

Straika huyo ambaye ana asili ya Tanzania alibadili uraia na kuwa Mrundi ambapo tayari ameanza mazungumzo na uongozi wa Stand, japokuwa jina lake bado limewekwa kapuni.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Mwenyekiti wa Stand, Aman Vincent alikiri juu ya kuwepo kwa mpango huo.

“Ni kweli tupo katika mazungumzo naye, lakini taarifa nyingine juu yake hatuwezi kuzisema kwa sasa kwa kuwa bado mapema,” alisema Vincent.   

Wakati huohuo, imefahamika kuwa zawadi ya basi aina ya Coaster waliyopewa Stand United, juzi Jumatano na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele, lina thamani ya shilingi milioni 48.

Mwenyekiti wa Stand, Amani Vincent amesema: “Basi hilo lina thamani ya shilingi milioni 48, litatusaidia sana tutakapoanza ligi, tunamshukuru sana mbunge wetu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic