July 1, 2014



Wachezaji watano wameombewa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) ili waweze kucheza mpira wa miguu nchini na nje ya Tanzania.


Mmoja wao ni kiungo wa Abdulhalim Humoud kutoka Simba ambaye Sofapaka ya Kenya imemuombea kibali cha kukipiga nchini humo.

Wengine ni Crispine Odulla (Coastal Union) na Haji Ugando (Mbagala Market FC) wameombewa ITC na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) ili wakacheze nchini humo katika klabu za Bandari FC na Nakuru All Stars.

Vilevile TFF imemuombea ITC mchezaji Ismaila Diarra kutoka nchini Mali ili aweze kujiunga na timu ya Azam FC. TFF inafanyia kazi maombi hayo, na mara taratibu zote zitakapokamilika itatoa ITC hizo kwa wachezaji wanaokwenda nje ya Tanzania.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic