July 1, 2014



Timu ya Taifa (Taifa Stars) inacheza mechi ya kirafiki na Botswana leo (Julai Mosi mwaka huu) kuanzia saa 9 alasiri kwa saa za huko.


Mechi itakayofanyika Uwanja wa Taifa jijini Gaborone ni sehemu ya maandalizi ya Taifa Stars kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kurejea nchini Julai 6 mwaka huu kuendelea na programu nyingine kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji.

Wakati huo huo, kutakuwa na utaratibu maalumu kwa waandishi wa habari za michezo kwa ajili ya kuripoti mechi ya Stars dhidi ya Msumbiji. Hivyo, vyombo vya habari vinatakiwa kutuma majina mawili ya waandishi watakaoripoti mechi hiyo. Mwisho wa kupokea majina hayo ni Julai 8 mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic