Waamuzi
wa mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Afrika Kusini
(Amajimbos) wanawasili leo (Julai 15 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Mechi
hiyo itafanyika Ijumaa (Julai 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex
uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam na itachezeshwa na waamuzi hao kutoka
Shelisheli. Kiingilio cha mechi hiyo ni sh. 2,000 tu.
Waamuzi
hao ambao wanawasili saa 2.05 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ni Allister
Barra, Gerard Pool, Jean Joseph Felix Ernest na Nelson Emile Fred.
Kamishna wa mechi
hiyo Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar pia anawasili leo saa
2.05 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.








0 COMMENTS:
Post a Comment