Semina
na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa waamuzi wa
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na baadhi ya wale wa daraja la
kwanza wenye kiwango cha juu (elite) itafanyika jijini Dar es Salaam.
Waamuzi
30 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watashiriki kwenye semina hiyo
itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Julai 21 hadi 26 mwaka
huu.
Mkufunzi
wa FIFA kwa Kanda ya Kusini mwa Afrika, Carlos Henriques kutoka Afrika Kusini
ndiye atakayeendesha semina hiyo akisaidiwa na Watanzania Charles Mchau kutoka
Kilimanjaro, Juma Ali David (Zanzibar), Joan Minja (Dar es Salaam) na Riziki
Majala (Pwani).
Waamuzi
na waamuzi wasaidizi wa FIFA watakaoshiriki semina hiyo ni Ferdinand Chacha
(Mwanza), Hamisi Chang’walu (Dar es Salaam), Israel Mujuni (Dar es Salaam),
Jesse Erasmo (Morogoro), John Kanyenye (Mbeya), Josephat Bulali (Zanzibar),
Kinduli Ali (Zanzibar), Oden Mbaga (Dar es Salaam), Ramadhan Ibada (Zanzibar),
Samwel Mpenzu (Arusha) na Waziri Sheha (Zanzibar).
Kwa
upande wa waamuzi wa daraja la kwanza ni Abdallah Kambuzi (Shinyanga), Agnes
Pandaleo (Arusha), Ahamada Simba (Kagera), Arnold Bugado (Singida), Charles
Simon (Dodoma), Dalila Jafari (Zanzibar), Frank Komba (Pwani), Helen Mduma (Dar
es Salaam), Issa Bilali (Zanzibar) na Issa Haji (Zanzibar).
Wengine
ni Janeth Balama (Iringa), Jonesia Rukyaa (Kagera), Lulu Mushi (Dar es Salaam),
Martin Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma), Mbaraka Haule (Zanzibar),
Mfaume Ally (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga) na Soud Lila (Dar es Salaam).
Washiriki wa
semina hiyo na wakufunzi wanatakiwa kuwasili jijini Dar es Salaam, Julai 20
mwaka huu.








0 COMMENTS:
Post a Comment