Kweli Mario Balotelli haishi vituko, tayari ameanza mazoezi na Liverpool, lakini vituko kama kawa.
Balotelli ametumia zaidi ya
dakika moja eti akisumbuka kuvaa bib ya mazoezi, wakati huo wenzake wakiendelea
na mazoezi.
Lakini kama hiyo haitoshi,
ingawa ndiyo siku ya kwanza akiwa na wenzake, tayari ameanza utani kwa
kuangushana na Kolo Toure.
Hofu ni moja, Balotelli
haeleweki, mara utani, mara ageuke ‘shoziniga’. Mashalah yake ni shiiiida.
Wakati Liverpool ikiendelea
na mazoezi, mashabiki wanaoishi nyumba jirani walishindwa kujizua baada ya
kupanda ukuta ili washuhudie kama ni kweli Balotelli yuko mazoezini.
0 COMMENTS:
Post a Comment