August 28, 2014




Emmanuel Okwi amesema ameamua kuomba kuichezea Simba baada ya Yanga kumtema katika usajili wa msimu mpya.

Okwi ameiambia SALEHJEMBE kwamba ameamua kuomba kurejea Simba akiamini anaweza kuwa na msaada.
“Yanga wameniacha, nikachukua uamuzi wa kurudi Simba na kuomba kuichezea nao wamenikublia.
“Najua Yanga wamenishitaki TFF au Fifa, nitaendelea kulishughulikia suala hilo wakati nikiwa naitumikia Simba.
“Nashukuru kwa kuwa wamenipokea kwa mikono miwili,” alisema Okwi akionyesha kujiamini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema wamemchukua Okwi baada ya kuandika barua kuomba arudi.
“Tumempokea baada kuipokea barua yake na kuijadili, kwa kuwa Yanga wamemuacha na hata FIfa inasisitiza wachezaji kupata nafasi ya kucheza ili kuepusha kuua vipaji vyao, tumeamua kuwa naye,” alisema Hans Poppe. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic