August 8, 2014


KISIGA


Jezi namba 10 ya Simba imeingia kwenye mgogoro kwa sasa kwamba nani ana jukumu la kuivaa jezi hiyo baada ya wachezaji watatu kikosini hapo kila mmoja kutaka kuitumia msimu ujao.


Simba ina wachezaji watatu ambao kila mmoja anajiona anastahili kuivaa ambao ni Shabani Kisiga aliyetokea Mtibwa Sugar na Ibrahim Twaha ‘Messi’ huku Mkenya Paul Kiongera anayetarajiwa kumwaga wino Msimbazi naye pia akitoa rai ya kuiomba jezi namba 10.
TWAHA

Msimu uliopita, jezi hiyo ilikuwa ikitumiwa na Uhuru Selemani, lakini sasa ameamua kubadili na kutumia namba saba.

Chanzo cha ndani kutoka Simba kimesema, Twaha ameing’ang’ania jezi hiyo na hataki kuiachia kwa kigezo kuwa aliwahi kuiomba kabla ya Kisiga, ambapo jana pia Twaha ndiye aliyekuwa ameivaa katika mazoezi ya asubuhi.

Gazeti hili lilipomuuliza Kisiga juu ya sakata hilo, alisema: “Kuna listi tayari imeandikwa na inaonyesha mimi ndiye nastahili kuvaa namba 10.”

Alipoulizwa Meneja wa Simba, Nico Nyagawa, alisema jezi hiyo itavaliwa na Kisiga na kusisitiza kuwa Twaha aliivaa mazoezini tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic