August 12, 2014



Kocha Zdravko Logarusic alipiga picha na kikosi cha Simba, pembeni akawepo Rais wa klabu, Evans Aveva.

Lakini hakujua kwamba saa chache baadaye, Aveva angetangaza kumtimua kazi.
Picha hiyo ya kikosi ilikuwa ni katika mechi ya kirafiki dhidi ya Zesco ambayo Simba ililala kwa mabao 3-0.
Jioni ya siku iliyofuata, Aveva ndiye alitangaza kufutwa kwake kazi ikiwa ni baada ya kamati ya utendaji kukaa.
Katika picha hiyo, unawaona Aveva na Loga ndiyo wenye suti nyeusi na wanapendeza kweli.
Halafu siku ya pili, urafiki wao, kwisha kazi. Picha hiyo inatoa funzo kwamba katika maisha, haujui kilicho mbele yako.
Kingine kinachovutia katika picha hiyo, Loga alipiga picha na wachezaji watatu aliowahi kufanya nao kazi Gor Mahia ya Kenya. Kwanza ni Donald Musoti, Ivo Mapunda na Modo Kiongera.
Lakini katika michezo, kuachishwa kazi na hasa kwa kocha wa soka, si jambo la kushangaza.
Wanasema kocha anaajiriwa ili atimuliwe. Ndiyo mambo ya soka

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic