WACHEZAJI WA STOKE CITY WAKIMPONGEZA SHUJAA MAME BIRAM DIOUF BAADA YA KUFUNGA BAO HILO PEKEE LA MCHEZO HUO. |
Mabingwa wa England, Manchester City wameanza kuonja joto ya jiwe wa
Ligi Kuu England baada ya leo kulala kwa bao 1-0.
Stoke City ambao waliinyanyasa Man City msimu uliopita, leo ‘wameifanyia
mbaya’ kwa kuichapa kwa bao 1-0 tu.
Mame Diouf ndiye alikuwa shujaa wa Stoke City waliokuwa nyumbani baada
ya kuwapangua viungo na mabeki wa wageni wao kabla ya kupachika bao akipiga
mpira uliompita kipa Joe Hart katikati ya miguu yake, unaweza kusema topo.
Juhudi za Man City kutaka kuchomoa 'kashfa' hiyo ziligonga mwamba.
0 COMMENTS:
Post a Comment