August 11, 2014



Simba iko katika hatua nzuri ya mazungumzo na Patrick Phiri na huenda akatua nchini ndani ya siku tatu kuanza kazi.
Phiri raia wa Zambia anatarajia kutua nchini kuchukua nafasi iliyoachwa na Zdravko Logarusic ambaye ametimuliwa na uongozi wa Simba baada ya kutoridhika namwenendo wake.
Logarusic raia wa Croatia anatarajia kuondoka nchini kurejea kwao na Phiri aliyewahi kuinoa Simba kwa vipindi vitatu tofauti, yuko katika hatua za mwisho kutua nchini.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza, makocha kadhaa wametuma wasifu wao kuwania kazi ya Loga.
Lakini uongozi wa Simba uliwaingiza fainali Phiri na Milovan Cirkovic lakini Mzambia akaonekana kukubalika na wajumbe wengi wa kamati ya utendaji.
“Mjadala ulianza baada ya kuona Loga ataondoka, mara moja Phiri amepata nafasi ya kwanza baada ya kumzidi Milovan na amekubali kuja, kuna mambo madogo ya kumalizia,” kilieleza chanzo.
“Lakini kuna mambo madogo ya kumalizia na yakikubalika, Ijumaa au Jumamosi atakuwa Dar kuungana na Matola ambaye anakuwa bosi kwa muda.”
Phiri ni kati ya kocha kipenzi cha Wanasimba na amekuwa akikubalika kutokana na kazi yake nzuri. Amewahi kuwa Kocha Mkuu wa Zambia ‘Chipolopolo’ aliyoipeleka hadi Kombe la Mataifa Afrika iliyofanyika nchini Ghana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic