August 8, 2014


 Shabiki mmoja ‘blood’ yaani, damu ile mbaya wa Simba, ametoa kali baada ya kuibuka kwenye mazoezi ya timu hiyo na mavazi ya magunia.

Shabiki huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 50 hadi 55, alikuwa amevaa shati, suruali na kofia za magunia, lakini zilizoshonwa kwa unadhifu mkubwa.

Alipofika mazoezini shabiki huyo alionyesha ni mwenye furaha na alikuwa akimsubiri Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic.
Loga alipowasili kwenye Uwanja wa Boko Veterani na kumkuta shabiki huyo, mara moja akampa nafasi, wakapiga picha pamoja.
Lakini Loga pia alionekana kuvutiwa na vazi la shabiki huyo la magunia ambaye alimpongeza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic